HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ISAAC ABRAHAMU SEPETU
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mwili wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu utafikishwa nyumbani kwake eneo la Sinza Mori lililoko jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne October 29, 2013 kuanzia saa sita za mchana na mwili huo utaanza kuagwa kwenye mida ya saa nane za mchana na baada ya kuagwa mwili huo utafanyiwa maandalizi ya kusafirishwa kwenda Zanzibar siku ya Jumatano asubuhi tarehe 30, October 2013 na mwili wa marehemu ukifika Zanzibar, Unguja utapelekwa kanisani kwa ajili ya maombi pia utapumzishwa kwenye makazi yake ya daima eneo la Mbozini, Unguja siku ya Jumatano October 30, 2013

Balozi David Kapya akisaini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake eneo la Sinza Mori jijini Dar es salaam leo Jumatatu October 28, 2013
Mke wa marehemu akiwa kwenye majonzi
Wema Sepetu akiwasiliana na ndugu na jamaa kwenye msiba wa baba yake marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 28, 2013
Mtoto wa maheremu na pia msemaji wa familia Aman Isaac Sepetu akizungumza na vyombo vya habari leo nyumbani kwa marehemu
Balozi
David Kapya akibadilishana mawazo na ndugu, jamaa na marafiki kwenye
msiba wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo nyumbani kwake maeneo
ya Sinza Mori
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba
Balozi
Isaac Abraham Sepetu alizaliwa October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora
ila alikulia Zanzibar na alikuwa ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti
yanamfika
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alipata elimu yake ya
msingi na sekondari katika shule ya St.joseph’s kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar mnamo mwaka 1952 hadi 1963, vilevile
aliweza kujiunga na chuo kikuu huko Berlin nchini Ujerumani mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya Uchumi,
Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa
ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza na kijerumani.
KAZI
Alianza kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972
kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ikulu. Baada ya hapo mwaka
1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya Nje katika serikali ya Muungano Zanzibar, mnamo
mwaka 1977 hadi 1979 Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji, Ilipofika mwaka 1979 hadi
1982 alikuwa Waziri wa Utalii na Maliasili .
Marehemu Balozi Sepetu
mwaka 1982 hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Moscow
na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa nchi ya Zaire, Kinshasa
Katika Serikali ya Mapinduzi
Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Mipango pia
alikuwa Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na pia alikuwa Katibu ,
Kamati ya Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa bunge la Afrika ya
Mashariki
Uzoefu wa Kisiasa
Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi
No comments: