Dkt. Sengondo Mvungi Akifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kujeruhiwa vibaya
Dkt.
Sengondo Mvungi, akiwa kwenye gari la kubeba wagonjwa, baada ya kufikishwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akihamishiwa hapo kutoka Hospitali ya
Tumbi, Kibaha Jumapili Novemba 3, 2013.
Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania (CRC), Dkt. Sengondo Mvungi.Picha zote na Khalfan Said
KAMISHNA
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania (CRC), Dkt. Sengondo Mvungi,
amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani na usoni, baada ya kukatwa
mapanga, nyumbani kwake, Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya jiji, majira ya
saa sita usiku Jumamosi Novemba 2, 2013.
Kwa
mujibu wa taarifa za ndugu na polisi, Dkt. Mvungi ambaye pia ni
Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, mkoani Pwani,
alicharangwa mapanga, baada ya kutaka kujua nini kilichokuwa kikiendelea
kufuatia mabishano baina ya mkewe na watu hao ambao walitishia kumuua
endapo asingewapa fedha.
Taarifa
zinasema, watu hao sita wengine wakiwa nje ya nyumba kwa nia ya
kujihami endapo wangevamiwa na majirani, walivamia nyumba hiyo yenye
ghorofa moja, na kumkuta mkewe Dkt. Mvungi wakati huo Dkt. Mvungi akiwa
kwenye chumba tofauti katika nyumba hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo, wavamizi walipoona mke wa Dkt. Mvungi
anachelewa kutekeleza maagizo yao, walifyatua baruti na hapo Dkt. Mvungi
akajaribu kuelekea kulikotokea mlio huo na ndipo alipokutana na mapanga
ya kichwani na usoni.
Uchunguzi
wa awali wa polisi umeonyesha kuwa tukio hilo ni la kihalifu, kwani
watu hao ambao kwa sasa wanatajwa kama majambazi, waliiba fedha, simu na
laptop, hali inayoonyesha wazi kuwa nia yao ilikuwa ni kutekeleza wizi.
Dk. Mvungi aliwahi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi
No comments: