Ads Top

PICHA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

  Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Mhe. Edward Lowasa,(kulia) akibadilshana mawazo na Wabunge wa CHADEMA, Mbunge wa Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (katikati) na Said Alfi, wa Mpanda mjini walipokutana nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma mara baada ya kuahirishwa kikao cha bunge kilichojadili kwa kina na kuazimia kuundwa kwa kamati teule ya bunge ili kufutilia ukiukwaji mkubwa wa sheria uliofanywa na waliosimamia na kuendesha zoezi oparation tokomeza ujangili.
 Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM,Mkoa wa Dar es salaam,Abasy Mtemvu (kulia) amabaye pia ni Mbunge wa Temeke, na Idd Azan (kushoto) ambaye pia ni Mbunge wa Kinondoni wakifurahia mchakato wa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma walipokutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama(katikati) kwenye viwanja  vya bunge.
 Wabunge wa CCM,Kangi Lugola (kulia) wa Jimbo la Mwibara,na Jenista Mhagama (katikati) wa Jimbo la Peramiho,wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto) walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma bunge linaendelea na mkutano wa 13 mjini humo ambapo hoja mbali mbali zinajadiliwa.
 Waziri wa Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samweli Sitta, (kulia) akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega CCM, Dk,Hamis Kigwangallah, walipokutana ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Ddodoma,ambako mkutano wa 13 wa bunge hilo unaendelea kujadili hoja mbali mbali za Serikali na zile za wabunge,ikiwamo ya vipaumbele vya maendeleo ya Taifa na ile ya mapungufu yaliyojitokeza wakati wa kutekelezaji wa zoezi la oparation ya tokomeza ujangili inayoendelea nchini.
 Naibu Waziri wa Fedha na uchumi, Saada Mkuya Salum, (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Peramiho,CCM, Jenista Mhagama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge walipokutana ndani ya ukumbi wa bunge, wakati wa mjadala wa vipaumbele vya maendeleo ya Taifa, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mahusiano na uratibu Stephen Wasira.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Chalres Kitwanga, (kushoto) akijadiliana jambo na Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama (kulia)Jimbo la  Peramiho na William Ngeleja (nyuma kulia) wa Jimbo la Sengerema, walipokutana ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma ambako bunge hilo linakutana katika mkutano wake wa 13.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.