TAARIFA KWA UMMA KUFUATIA KUTEULIWA KWA MHESHIMIWA RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUWA BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO DUNIANI KUPITIA SHIRIKA LA GAVI
 
 
JAMHURI 
YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA KUFUATIA KUTEULIWA KWA MHESHIMIWA 
RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUWA BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO 
DUNIANI KUPITIA SHIRIKA LA GAVI
Serikali
 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi 
uliofanywa na Shirika la Global Alliance for Vaccines and 
Immunizations (GAVI) kwa  kumteua Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
 
Rais  Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
kuwa Balozi wa Heshima wa Chanjo Duniani. Kwa niaba ya Serikali, Wizara 
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa niaba yangu 
binafsi napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. 
Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi huu.
Ndugu wananchi, 
Kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari  Rais wetu 
mstaafu wa awamu ya nne (4) Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa 
kuwa BALOZI WA HESHIMA WA CHANJO DUNIANI kupitia shirikia laGlobal  
Alliance for Vaccines  and  Immunizations (GAVI) mnamo tarehe 
31Januari,2016 nchini Ethiopia.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda 
kuchukua fursa hiikuungana na shirika la GAVI pamoja na wananchi wote 
wa Tanzaniakumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi 
huo. Kuteuliwa  kwake kuwa Balozi wa heshima kwenye masuala ya chanjo, 
kuna maana ya kuwa,atakuwa mhamasishaji wa  wakuu wote wa nchi  
za Afrika na dunia kwa ujumla kuhakikisha  wanaweka kipaumbele katika  
upatikanaji wa huduma za afya hususan masuala ya chanjo.
Katika muda wote wa uongozi wake Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete 
alitoa kipaumbele  katika  masuala ya afya ya uzazi  na  
mtoto  likiwemo suala la chanjo   na  kuhakikisha wanawake 
na watoto  wanapata huduma ipasavyo.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja 
na Watanzania wote tumefarijika sana kwa uteuzi huo, kwani pamoja na 
juhudi hizo, amekuwa  ni Mwenyekiti mwenza wa Jopo la watu mashuhuri 
la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  juu ya uboreshaji 
wa malengo ya  Maendeleo  endelevu.(Sustainable Development 
Goals)
Aidha,Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alishiriki katika mkutano 
mkubwa wa GAVI uliofanyika mnamo tarehe 26 hadi 27Januari  2015 nchini 
Ujerumani na kueleza dhamira yake na ya nchi kwa ujumla katika kushiriki 
kikamilifu kupunguza kiwango kikubwa cha maradhi na vifo vitokanavyo 
na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Jakaya 
Mrisho Kikwete,Tanzania iliweza kuongeza kiwango cha  utoaji wa 
huduma za chanjo hadi  kufikia  wastani wa zaidi ya asilimia 
95 ikiwa ni zaidi ya lengo la Kimataifa la  asilimia  90.Tunaami 
kuwa mafanikio haya yamechangia Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete 
kupewa heshima hiyo.
Historia inaonyesha kuwa kwenye miaka ya sabini watoto wengi walipoteza 
maisha yao kutokana na magonjwa yanayozuilika  kwa chanjo.Wengi 
wetu ni mashahidi wa milipuko na vifo vilivyotokana na ugonjwa wa surua 
kipindi hicho. Wodi nyingi katika Hospitali zetu zilitengwa na zilijaa 
watoto waliougua surua na ugonjwa wa pepo punda.  Aidha, watoto 
wengi  walibakia na ulemavu wa viungo, ulemavu wa kutoona, ulemavu 
wa kutosikia,  na mtindio wa ubongo kutokana na athari za magonjwa 
ya polio na  surua.
Juhudi za Serikali katika kukabiliana na magonjwa yanayozuilika kwa 
chanjo zimeleta mafanikio makubwa. Kwa mfano, magonjwa ya ndui na pepopunda 
kwa watoto wachanga yametoweka,pia tumeshuhudia wodi za surua zikifungwa, 
na vifo vitokanavyo na surua kupungua kwa kiasi kikubwa.Aidha Tanzania 
imekwisha thibitishwa kuwa ni miongoni mwa nchi zilizotokomeza ugonjwa 
wa Polio duniani. Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali  
kuwekeza katika chanjo.
Imethibitika kuwa chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza magonjwa  
na kupunguza vifo vya watoto, hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia zetu na Taifa kwa ujumla lingetumia 
katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. 
Rejea za kitaaluma zimethibitisha kuwa chanjo huzuia takribani vifo 
Milioni 2 hadi 3 kila mwaka kutokana na maradhi yanayozuilika  
kwa chanjo duniani. Nchini Tanzania,  mwaka 2004, vifo vya watoto 
chini ya miaka mitano vilikuwa 112 kati ya vizazi hai 1,000 na viliendelea 
kupungua hadi vifo 81 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2010.
Mojawapo ya mikakati ya Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika 
kipindi chake cha uongozi ilikuwa ni kufikia malengo ya maendeleo ya 
Milenia. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa (UN Inter Agency 
Report for child mortality estimates), Tanzania ilifanikiwa kufikia 
lengo la Millenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto walio na umri 
chini ya miaka 5 kutoka vifo 81 hadi vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 
mwaka 2013. 
Tunafahamu kuwa Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ana kazi kubwa 
mbele yake ya kuhakikisha nchi zote za Afrika na Dunia kwa ujumla zinafikia 
kiwango cha wastani wa asilimia 90 wa chanjo kwani, hadi sasa,  
bado kuna nchi ambazo bado zina kiwango cha wastani wa asilimia 50.
Ni faraja yetu kubwa  kuwa Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete 
ataendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha  upatikanaji wa huduma 
za chanjo barani  Afrika na dunia kwa ujumla na hivyo kuokoa maisha 
ya watoto.
Tunamtakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu hayo makubwa 
kidunia,na kumuahidi ushirikiano wetu.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
1.3.2016
 
 
 
 
 
 
 
No comments: