NDUGU WA WAFANYAKAZI WA MSCTN WAMLILIA MAGUFULI
Na antony Sollo, Mwanza
KUFUATIA Mgogoro mkubwa uliokuwa ukifukuta kati ya wafanyakazi wa Kampuni ya
Mwanza SateliteCables Television Network Limited (MSCTN ) inayotoa huduma za
usambazaji wamawasiliano ya TV katika
maeneo mbalimbali Jijini Mwanza dhidi ya mwajiri wao ndugu wa wafanyakazi hao
wamemuomba JPM awasaidie kwa kuingilia kati Mwana Halisi linaweza kuripoti.
Akizungumza na MwanaHalisi mmoja wa ndugu wa wafanyakazi hao
amelalamikia ukiukwaji wa Sheria na Haki uliotekelezwa na mwajiri wa vijana hao
huku akidai kuwa kulikuwa na ukandamizaji mkubwa wa Haki.
Imeelezwa kuwa wafanyakazi hao kabla ya kufanyiwa unyama huo
Mwajiri wao aliwafungulia mashitaka polisi akiwatuhumu kufanya fujo na baadaye.
kuwataka kukabidhi funguo za Ofisi bila kuwapatia barua ya
kuacha kazi jambo ambalo lilisababisha mgogoro huo kuwa mkubwa.
Wafanyakazi waliokuwa na mgogoro na mwajiri wao ni Samora
Ernest,Waryoba Finias na Antony Lucas
wanadai ambapo kwa taarifa zilizothibitishwa na ndugu yao huyo ni kwamba
wafanyakazi hao walikamatwa na polisi Machi 22, mwaka huu majira ya saa
2:00walipokwenda ofisini na kisha
wakafunguliwa kesi ya kufanya fujo na mwajiri wao huku wakiendelea kupewa
vitisho kuwa atahakikisha kuwa iwapo hawataacha kudai haki zao atawafunga jela
kwa madai kwamba yeye yuko vizuri na watendaji wa jeshi la polisi na vyombo vya
Maamuzi.
Uchunguzi uliofanywa na MwanaHalisi umebaini kuwa sababu ya
kufunguliwa kesi kwa vijana hao ni
kutokana na siri kubwa waliyokuwa nayo wafanyakazi hao juu ya tuhuma za Kampuni
hiyo kukwepa kodi kwa muda mrefu ambapo
walilalamikia kitendo hicho kwa wafanyakazi wa Serikali Jijini Mwanza lakini
Mwajiri alitumia kila njia kuhakikisha wanapotea uraiani.
Katika madai yao,wafanyakazi hao walikuwa wakilalamikia
mapunjo ya mishahara na kunyimwa mkataba wa ajira bambapo baada ya kuonyesha
msimamo wao walitishiwa kuwa wangebambikiwa kesi na mwajiri wao ili kupoteza
ushahidi wa madai yao ambapo baada ya vitisho hivyo walipeleka malalamiko yao
kwa Waziri wa Kazi Ajira Vijana na
Walemavu lakini hata baada ya mwajiri kupewa agizo na waziri hakutekeleza
chochote ya kutekeleza adhima yake ambapo hadi sasa vijana hao wako Magereza
wakitumikia kifungo.
MwanaHalisi lilipata kuiona nakala iliyokuwa na maelekezo
yaliyotolewa na Kamishna
MwanaHalisi lilishuhudia jalada la kesi namba
MW/RB/2526/17 lililofunguliwa dhidi wafanyakazi hao wakituhumiwa kufanya fujo ambapo kesi
hiyo ilifunguliwa Kituo kikuu cha polisi kati Jijini Mwanza.
“yote haya walifanyiwa
na mwajiri ili kupoteza ushahidi kutokana
madai yao zote hizi zikiwa ni njama za makusudi ili kuwanyamzisha,”alisema ndugu wa wafanyakazi
hao.
Kampuni ya MSCTN inadaiwa kuwanyima wafanyakazi baadhi
mikataba ya ajira, kuwapunja mishahara, kutowaandikisha kwenye mifuko
ya hifadhi ya jamii na hivyo kusababisha mgogoro ambao
waliufikisha kwa
Waziri wa Bunge, Sera, Vijana, Kazi, Ajira na walemavu ambapo
Katibu Mkuu wa wizara hiyo alimwagiza Kamishna wa Idara ya Kazi mkoa wa Mwanza kufanya uchunguzi wa madai ya wafanyakazi
hao nakuchukua hatua stahiki ili walipwe stahili zao.
“Kilichofanyika ni usanii , eti wafanyakazi walikuwa
wanalazimishwa wakubali kusaini mikataba mipya bila kulipwa mapunjo yao ya
nyuma na kwamba walikuwa wakilipwa mishahara pungufu ya kima cha chini cha mshahara wa serikali
muda mrefu, baada ya malalamiko yao kuyawasilisha sehemu
mbalimbali mwajiri wao aliamua kutengeneza mikataba feki na
kuwalazimisha kuisaini jambo ambalo si sawa” alisema ndugu yao huyo kwa
sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
MwanaHalisi lilimtafuta Mkurugenzi wa Mwanza Cables Ridhiwani
Kanji ambaye hata baada ya kutakiwa kueleza juu ya tuhuma hizo hakuwa tayari
kukubali ambapo alikanusha tuhuma hizokuwa si za kweli na kwamba wafanyakazi
hao waligoma kukaguliwa ili kubaini maendeleo ya matawi ya kampuni hiyo
yaliyoko katika maeneo mbalimbali jijini Mwanza.
Kwa upende wake Afisa Kazi mkoani Mwanza Joshua Malongo
alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo alikiri kupokea maagizo ya Katibu Mkuu
Februari 2 mwaka huu na kufanya uchunguzi kama alivyoelekezwa ambapo katika uchunguzi aliofanya alibaini kuwepo
kwa ukweli katika malalamiko na madai ya wafanyakazi hao kuwa ni ya kweli na hivyo alimwandikia barua
ya utekelezaji mwajiri wao.
“ Ni kweli nilipokea maagizo hayo na kuyafanyia kazi na
tunapozungumza tayari nimemwandikia mwajiri wao barua ya utekelezaji ikiwa ni
pamoja na kuwapa mikataba ya ajira na kuwalipa kiwango cha mshahara wa sh.
150,000 kwa mwezi kama agizo la Serikali linavyoelekeza ” alisema Joshua
MwanaHalisi lilifanikiwa pia kupata nakala ya barua yenye kumb Na MWA/AD/M/43/5
ya 14.02.2017 ya Utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na 6 na
Sheria ya Taasisi za kazi na 7 ya 2004 ambapo hata hivyo gazeti hili limebaini
kuwa hata baada ya kupelekewa barua hiyo mwajiri hajafanya utekelezaji
wowote.
Alipotakiwa kuzungumzia kutotekelezwa kwa maagizo ya Wizara
ya Kazi Afisa Mwajiri wa MSCTN Fredrick Kilassa alisemakampuni hiyo inafanya
shuguli zake kihalali licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro na wafanyakazi hao
tangu Desemba 2016.
“Ninachokifahamu mimi uongozi wa kampuni hiyo uliamua kufanya
ukaguzi wa miradi katika matawi mbalimbali ambayo yanatoa huduma lakini
wafanyakazi wetu hawa waligoma kukaguliwa na ndiyo chanzo cha mgogoro wetu.
Kuhusu tuhuma za kukwepa kodi na mapato ya Serikali MwanaHalisi lilifuatilia
katika mamlaka ya Mapato TRA na kukutana na Afisa Elimu kwa mlipa Kodi Mkoa wa
Mwanza Lutufya Mtafya ambaye pamoja na mambo mengine alisema kuwa amepokea
taarifa hizi hata kabla ya gazeti hili kufika hapo.
“tumepokea malalamiko haya muda mrefu ila tuko katika
harakati ya kuunda timu itakayokwenda kufanya uchunguzi, iwapo mwajiri wa
Kampuni ya MSCTN anakusanya fedha kwa kutumia mashine moja ya EFD wakati ana
matawi matano ni kosa na hivyo tutafanya uchunguzi ikibainika tutachukua hatua
za kinidhamu dhidi yake”.alisema Mtafya.
Kufuatia njama za kuwabambikiza kesi vijana hawa hadi sasa
wamehukumiwa kifungo katika gereza la Butimba jijini Mwanza ambapo wamemuomba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli aingilie kati sakata hili
ili kuwaokoa wanyonge wanaokandamizwa na waajiri wanaokiuka Sheria za nchi.
MWISHO
No comments: