WALEMAVU WALISHIKA PABAYA JESHI LA POLISI
Na Antony Sollo - DSM.
Kufuatia matumizi ya
nguvu yaliyofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi juni 16 mwaka huu, Viongozi wa
Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi kwa watu wenye ulemavu
wametoa tamko rasmi huku wakilipa jeshi hilo siku saba kuwaomba radhi
vinginevyo watalifikisha jeshi hilo Mahakamani wakiwatuhumu kwa makossa
mbalimbali ikiwemo kuharibu mali,shambulizi na udahalilishaji kwa watu wenye
ulemavu.
Wakizungumza na
Waandishi wa Habari wadau wa Haki za Binadamu kikiwemo Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu LHRC wamelaani vikali matumizi ya nguvu iliyopitiliza yaliyofanywa
na jeshi la polisi Tanzania katika zoezi la kuzuia kilichodaiwa kuwa ni
maandamano ya watu wenye ulemavu katika eneo la Posta jijini Dar es salaam.
Akitoa Tamko kwa upande
wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Wakili Anna
Henga alisema kuwa,kundi la watu wenye ulemavu ni moja ya makundi maalumu
katika jamii kundi ambalo linahitaji ulinzi mkubwa ili kuhakikisha usalama na
mazingira mazuri.
‘Mbali na kuwekewa
ulinzi kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kundi hili la
walemavu nchini linahitaji kuhakikishiwa usalama maana nchi yetu imeingia
mikataba ya Haki za Binadamu ya Kikanda na Kimataifa, hivyo walemavu
wanastahiliheshima ya utu wao kama Binadamu wengine kwa hiyo kitendo cha
kuwapiga kuwaburuza na kuwadhalilisha na kuwaharibia nyenzo zao zinazowasaidia
katika shughuli zao ni matumizi mabaya ya nguvu pamoja na mamlaka dhidi ya kundi
hilo ’alisema Henga.
Kwa hiyo Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu LHRC Tunalaani kwa nguvu zote kitendo kilichofanywa
na jeshi la polisi dhidi ya kundi hili kinyume
na kifungu cha (4) cha Sheria ya watu wenye ulemavuya (2010) kanuni za msingi
juu ya watu wenye ulemavu na Haki zao.
Akihitimisha tamko la
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Henga alisema kuwa jeshi la Polisi
limefanya jambo ambalo linalokiuka kanuni na Sheria za nchi na kulitaka jeshi
hilo lifanye kazi zake kwa mujibu wa Sheria ili kulinda raia na mali zake kama
yalivyo makusudi ya kuanzishwa kwake.
‘Ifahamike kwamba watu
wenye ulemavu kwa muktadha huohuo wamewekewa kinga dhidi ya mateso kwa nafasi
yao kama kundi maalumu na pia kama kundi la binadamu wengine’alisema Henga.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Haki za Binadamu
na Maendeleo ya Kiuchumi kwa watu wenye ulemavu Daud Nyendo alisema kuwa jeshi
la polisi lijitathmini upya juu ya matumizi ya nguvu hasa kwa watu ambao
hawakuwa na silaha tena wakiwa ni kundi maalumu la walemavu kwa kuwaharibia
mali zao na kuwafedhehesha na kulitaka jeshi hilo liache matumizi ya nguvu
iliyopitiliza na kuwaomba Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam
wajitokeze hadharani kuomba radhi kwa
walemavu hao kwa namna yoyote na Taifa kwa ujumla wake na kwamba lisipofanya
hivyo litafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi.
Sanjari na hilo
Mkurugenzi huyo amelitaka jeshi la Polisi litoe fidia kwa walemavu hao
(waathirika) wa shambulizi hilo ambapo inakadiriwa kuwepo kwa uharibifu mkubwa
wa mali zao ikiwemo baiskeli za walemavu hao (30) simu mbili ambazo hata hivyo
thamani yake haikufahamika mara moja.
No comments: