EMIRATES YATOA HUDUMA KWA FAMILIA ZA KITANZANIA NA SINEMA- DAR ES SALAAM
Emirates imewapa baadhi ya familia za kitanzania ladha ya
ushindi wa usafiri wa anga wakati walipohudumia kundi la wazazi na watoto wao
katika moja ya sinema kali ya Despicable Me 3. Sinema mpya iliyotoka katika
anga ya dunia- karibia watoto 30 na wazazi wao na walezi walihudhuria uzinduzi
huo uliofanyika Mlimani City Mall IMAX tarehe 8 Julai 2017 kuangalia sinema
bora uliyovuta hisia za wengi ikifatiwa na chakula cha mchana sehemu hiyo hiyo iliyoandaliwa
na mwenyeji mkurugenzi wa Emirates Tanzania, Rashed Alfajeer. Emirates pia
ilipata uzoefu wa familia katika kutangaza ofa ya 50% katika daraja la uchumi
kati ya abiria 2 - 8 kusafiri wote katika sehemu 21 zilizopendekezwa kama
Uarabuni, Ulaya vile vile Marekani kusini na kaskazini. Hiyo ofa ni kati ya
tarehe 6 na 14 julai 2017 na za nje kati ya tarehe 6 julai na 10 Disemba 2017.
Rashed Alfajeer, Mkurugenzi Mkuu wa Emirates Tanzania
alisema: " Emirates ipo kwa ajili ya kutoa thamani kwa pesa na
wamejihakikisha kutoa huduma iliyo bora angani mpaka ardhini na hakuna tofauti
linapokuja swala la familia katika kusafiri. Kwa watoto, lazima wawekwe huru na
waburudike na kuwajali kwa kuwapa wigo mpana katika kuchagua sinema na programu
ili kukithi mahitaji yao".
Ofa hii maalum inatoa nafasi kubwa kwa familia kuwa na
likizo ya pamoja sehemu mbali mbali kwa gharama nafuu kwa muda uliowekwa tu na
kuongeza wakati wakisafiria na Emirates, familia itarajie kupata wigo mpana wa
program za watoto ikiwa na channeli 90 mahususi kwa ajili ya kuwaburudisha
watoto ikiwamo pamoja na sinema bora na programu za TV kutoka Disney, Cartoon
Network, Cbeebies Na Nickelodon na nyingine nyingi. Chakula pia upewa
kipaumbele sana pindi abiria wawapo angani kwenye Emirates. Watoto wenye umri
kati ya miaka 2 na 12 hupewa chakula maalum wakihudumiwa katika vyombo vya
kisasa wakiwa na staff pamoja na marubani. Wasafiri wenye ugunduzi wachache wanaweza
kupata marafiki wapya pindi wawapo safarini, kuna blanketi kwa ajili ya
kujifunika na kuweza kujiburudisha na majarida yanayokuja Dar Es Salaam kila
siku. Ndege ya EK 0725 inatoka Dubai saa 10:25 na kufika Dar Es Salaam saa
14:50. Ndege inayorudi EK 0726 inatoka Dar Es Salaam saa 16:45 na kufika Dubai
saa 23:20.
------------------------------MWISHO--------------------------
No comments: