EMIRATES YAONGEZA MUDA WA NAULI MAALUM ZA DUBAI NA OFA YA VIZA BURE. OFA HIYO PIA KUJUMUISHA USIMAMIZI WA MIZIGO NA MY EMIRATES PASS
DAR ES
SALAAM, TANZANIA, 12 JULY 2017, Emirates imeongeza muda wa ofa kwa
wasafiri kutoka Tanzania kwenda Dubai kwa ofa maalum ndani ya daraja la kawaida
na daraja la juu kwenye nauli ya kwenda na kurudi ambayo itaambatana na viza
bure, nafasi ya kuweka mzigo usiozidi kilo 23 na My Emirates Pass.
Ndani ya ofa hii maalum, Tiketi ya daraja la
kawaida kutoka Dar Es Salaam mpaka Dubai ni USD 399 na daraja la juu ni USD
1999. Ofa hiyo ya nauli inatengemea na uwepo wa nafasi, vigezo na masharti na
kwa muda ulioainishwa tu. Unaweza kutuma maombi ya kupata nafasi kati ya 11
Julai na 24 Julai wakati safari ni kati ya 11 Julai na 30 Novemba 2017. Gharama
ya tiketi inajumuishwa pia na kodi ya uwanja wa ndege.
Ikipigiwa kura na wasafiri kuwa chombo
maridhawa kwa kutoa huduma duniani mwaka 2017 katika kinyanganyiro cha
TripAdvisor Travelers' Choice Awards. Emirates pia inatoa ofa ya viza ya siku
30 ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (inatengemea na uthibitisho wa idara ya
uhamiaji), nafasi ya kuhifadhi mzigo isiozidi kilo 23 kwa daraja la kawaida na
mpaka kilo 32 kwa daraja la juu, vile vile My Emirates Pass inaweza kutumika
kwa ofa mbalimbali na kupata punguzo ndani ya Dubai.
My Emirates Pass ambayo inatumika mpaka 31
August 2017, inawapa wateja punguzo maalum katika mahotel na migahawa zaidi ya
120 yenye ubora duniani ndani ya Dubai. Pia kuna ofa mbalimbali katika nyanja
ya burudani, kutembelea shindano la gofu, kutembelea mbuga na sehemu maridhawa
ndani ya jiji la Dubai. Kuona ofa za My Emirates Pass tembelea www.emirates.com/english/offers/4221290/my-emirates-pass
Ukiwa Dubai kwenye mandhari tulivu, utafanya
manunuzi ya vitu vya hali ya kimataifa, kupata huduma kwenye migahawa mikubwa,
kupunga upepo kwenye fukwe tulivu na kuona majengo ya kila aina, Dubai inakupa
ladha ya kifamilia. Wageni wakiwa huko wanaweza kutumia My Emirates Pass
kufurahia vivutio vya jiji na sehemu maarufu kama Hifadhi ya Dubai na mwambao
ikiwemo na hifadhi tatu maarufu kama bollywood, Dubai Motiongate bila kusahau hifadhi
ya kwanza katika mkoa huu legoland park na legoland water park.
Jiji la Dubai pia ina ofa ya malazi
inayoendana na matumizi yako.
Katika kila ndege za Emirates wasafiri
watapata viburudisho vya program za television katika chaneli 2500 kutokana na
mahitaji yao ikiwemo ya kusikiliza na kuona kutoka sinema mpya, muziki na
michezo, pia bidhaa rafiki za kifamilia na huduma kwa watoto kama michezo,
chakula kwa watoto na sinema, kupewa kipaumbele kama familia na matumizi ya
bure ya kubebewa mzigo ndani ya uwanja wa Kimataifa wa ndege ya Dubai.
Kwa kuongezea, ili kupata utulivu wa kujihami
na bidhaa, wateja watapata ukarimu wa kimataifa toka kwa wahudumu wa kimataifa
kutoka kwenye safu yetu huku wakiburudika kwa vyakula vilivyoandaliwa kitaifa
na kimataifa na wapishi wetu kwa kutumia vyakula asili ikizindikizwa na aina
mbalimbali ya vinywaji
Emirates inasafiri mara moja kila siku kati
ya Dubai na Dar Es Salaam ikitumia Boeing 777. Kupata nafasi au kwa maelezo
mengine kuhusu tiketi, vigezo na masharti tafadhali tembelea www.emirates.com/tz, ofisi za
Emirates au mawakala wa Emirates.
No comments: