RAILA ODINGA AMEAPA KUENDELEA KUFANYA MAANDAMANO DHIDI YA UCHAGUZI WA UHURU KENYATTA AKISISITIZA KUWA UPINZANI HAUMTAMBUI
Odinga anasema kuwa
Nasa haitambui uchaguzi huo kwa kuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati pamoja
na kamishna aliyejiuzulu Roselyn Akombe walithibitisha kwa umma kuwa tume hiyo
haiwezi kusimamia uchaguzi ulio huru kutokana na misimamo ya kimapendeleo ya
baadhi ya makamishna katika tume hiyo.
Odinga ambaye alikuwa
akitoa mwelekeo wa upinzani kwa vyombo vya habari katika jumba la OKoa Kenya
jijini Nairobi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kulikuwa na
uingiliaji na uongezaji wa kura katika ngome za chama tawala cha Jubilee.
Anasema kwamba iwapo
uchaguzi huo utaruhusiwa na kutambulika utawavunja moyo Wakenya wengi na
hivyobasi kuwafanya kutoshiriki katika uchaguzi mwengine wowote.
Mr Odinga pia amesema
kuwa hawezi kuwaruhusu watu wawili wanaojigamba kuwa na uwezo kuharibu uhuru na
demokrasia ilipatikana.
Amesema kuwa iwapo
uchaguzi wa Uhuru utaruhusiwa kuna uwezekano kwamba ataingilia katiba na
kuongeza muhula wa kuongoza.
''Tutaendelea kufanya
maandamno kila mara'', alisema Raila Odinga.
No comments: