WAZIRI MPINA ATOA SIKU MBILI NG’OMBE 640 ZIREJESHWE KWA WAFUGAJI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Luhaga Mpina akiwa katika pori la akiba la Rukwa
Rukwati akiangalia baadhi ya ng’ombe waliokufa
wakiwa wanashikiliwa na Taasisi ya Rukwa Rukwati ambapo
jumla ya mifugo hiyo 692 1mekufa kati ya mifugo 1332 iliyokuwa
inashikiliwa .
Picha na Mpiga picha Wetu
Na
Antony Sollo - Katavi
October
7, 2017
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameupa
siku mbili Uongozi wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati kurejesha
mara moja ng’ombe wapatao 640 waliosalia ambao ni mali ya wafujaji
watatu kwa kuwa walikuwa wanashikiliwa kwa muda wa mwaka mmoja kinyume cha Sheria.
Waziri Mpina alitoa agizo hilo Oktoba 5 mwaka
huu wakati alipotembelea hifadhi hiyo iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani
Mlele Mkoa wa Katavi kwa lengo la kutatua mgogoro wa muda mrefu
baina ya wafugaji hao watatu na uongozi wa hifadhi hiyo.
Imeelezwa
kuwa ng’ombe wapatao 692 ambao ni miongoni 1,332
walioshikiliwa na kuzuiliwa katika Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa –
Lukwati kwa zaidi ya mwaka mmoja wamekufa kwa kukosa matunzo bora.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mpina alionyesha kushutushwa na taarifa iliyosomwa kwake na
Meneja wa Hifadhi hiyo,Paschal Mhina kuwa ng’ombe wapatao 1,332
waliovamia hifadhi walikamatwa na kushikiliwa kwa mwaka mmoja
na miezi tisa ambapo ng’ombe wapatao 692 wameshakufa na waliobakia ni 640
tu .
Mpina aliuagiza
uongozi wa Serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha unahakiki mifugo
hiyo na kuwakabidhi wenye mali na kwamba wale wote watakaobainika
kusababisha vifo vya ng’ombe hao waliokufa kwa uzembe wachukuliwe hatua
kali za kinidhamu na za kijinai .
“
Hakukuwa na sababu yoyote ile ya msingi ya
kuendelea kuishilikia mifugo hiyo baada ya wenye
mali hiyo kufungua mashitaka mahakamani ambapo katika
kesi ya awali watuhumiwa watatu ambao ndiyo wenye mali hiyo walifungua
mashataka katika Mahakama ya Wilaya
ya Mpanda ambapo mahakama hiyo iliamuru
itaifishwe na iwe mali ya Serikali”
alieleza .
Waziri
huyo alimtaka Meneja wa pori
la Akiba amwonyeshe hati
yoyote inayowapa mamlaka ya kuendelea
kuwashikilia ngombe hao wakati wafugaji walikuwa wanatuhumiwa
walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga kupinga
kutaifishiwa ngombe zao lakini
hakuweza kufanya hivyo.
Hata
hivyo imebainika kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ilitengua
hukumu iliyotolewa na Mahama ya Wilaya ya Mpanda na
kuamuru wafugaji hao watatu warejeshewe mifugo yao na faini
ya Sh 500,000/- walizotozwa .
Wafugaji
hao watatu ni pamoja na Shigela Mayunga , Charles Mtokambali na Keleja
Makuja .
“Nimesikitishwa sana
na kitendo cha Uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba la Rukwa
Lukwati kwa kuendelea kuishikilia mifugo hiyo ambapo idadi kubwa ya
mifugo hiyo imekufa kwa magonjwa nataka kujua kwa nini
mifugo hiyo iliendelea kushikiliwa ndani ya hifadhi hiyo huku
eneo hilo likiwa limetengwa maalumu kwa ajili ya wanyamapori na sio
ng’ombe” alihoji Mpina huku akionyesha hisia kali kufuatia ukatili
uliofanywa.
Kwa
upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Rukwa Rukwati
Mhina alieleza kuwa mifugo hiyo ilendelea kushikiliwa
kwa kile alichodai kuwa baada ya
uongozi wa hifadhi hiyo kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu
Kanda ya Sumbawanga.
Akijitetea
Mhina alisema kuwa ungozi wa hifadhi hiyo ulipewa maelekezo na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa waendelee kuitunza mifugo hiyo
kama sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo .
Kwa
upande wake , Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafugaji Tanzania Makoye Nkonosinema alisema kuwa mifugo
iliyokufa ikiwa mikononi mwa uongozi wa hifadhi hiyo
wataendelea kuidai.
Aidha
alitaka kupewa maelezo ya kina katika kipindi hicho chote ambacho ng’ombe
hao walikuwa wameshikiliwa ni ndama wangapi waliozaliwa .
Naye Ofisa
Utafiti wa Magonjwa ya Mifugo wa Mikoa wa
Katavi na Rukwa , Protus Reshola alisema kuwa idadi hiyo ya ng’ombe
iliyokufa ni kubwa sana kwamba imesababishwa na dosari kadhaa
ikiwemo waliokuwa wakiwachunga walikuwa sio wafugaji .
Aliongeza
kuwa kutopatiwa matibabu stahiki na kutokuwepo na josho kwenye hifadhi
hiyo kumesababisha ng’ombe hao kufa kutokana na ugonjwa wa homa ya
mapafu .
Mwisho
No comments: