NI KUHUSU NG’OMBE 640 KUREJESHWA KWA WAFUGAJI
Na
Antony Sollo - Katavi
14 Nov, 2017.
UONGOZI
wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati unadaiwa kupuuza agizo
lililotolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kuhusu kurejesha
mara moja ng’ombe wapatao 640 waliosalia baada ya Wafugaji waliokamatiwa
Mifugo hiyo kulalamika kwa Waziri Mpina wakati wa Ziara yake katika Bonde la
Ziwa Rukwa wilayani Mlele Mkoa wa Katavi kwa lengo la kutatua
mgogoro wa muda mrefu baina ya wafugaji hao watatu na uongozi wa hifadhi hiyo.
Mpina alitoa agizo hilo Oktoba 5 mwaka
huu
baada
ya kubaini kuwa Uongozi wa Hifadhi hiyo ulikuwa ukishikilia mifugo hiyo kinyume
na Sheria kwa muda wa mwaka mmoja.
Ilielezwa
kuwa,ng’ombe wapatao 692 ambao ni miongoni 1,332 walioshikiliwa na
kuzuiliwa katika Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati kwa
zaidi ya mwaka mmoja na kwamba walikufa kwa kukosa matunzo bora.
Kufuatia hali hiyo Waziri Mpina
alionyesha kushutushwa na taarifa iliyosomwa kwake na Meneja wa Hifadhi
hiyo,Paschal Mhina kuwa ng’ombe wapatao 1,332 waliovamia hifadhi
walikamatwa na kushikiliwa kwa mwaka mmoja na miezi tisa
ambapo ng’ombe wapatao 692 wameshakufa na waliobakia ni 640 tu.
Mpina aliuagiza uongozi wa
Serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha unahakiki mifugo hiyo na
kuwakabidhi wenye mali na kwamba wale wote watakaobainika kusababisha
vifo vya ng’ombe hao waliokufa kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kinidhamu
na za kijinai.
“ Hakukuwa na sababu
yoyote ile ya msingi ya kuendelea kuishilikia mifugo
hiyo hasa baada ya wenye mali kufunguliwa Mashitaka katika Mahakama
ya wilaya ya Mpanda ambapo mahakama hiyo iliamuru washitakiwa
walipe faini ya shilingi laki tano na mifugo yao itaifishwa na iwe mali
ya Serikali ambapo wafugaji hao walikata Rufaa katika Mahakama Kuu
Kanda ya Sumbawanga na na Mahakama hiyo kutengua uamuzi wa Mahakama ya Wilaya
ya Mpanda” alisema Mpina.
Kufuatiahali hiyo,Waziri Mpina
alimtaka Meneja wa pori
la Akiba amwonyeshe hati
yoyote inayowapa mamlaka ya kuendelea
kuwashikilia ngombe hao
wakati wafugaji walikuwa wanatuhumiwa
walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga kupinga
kutaifishiwa ngombe zao lakini hakuweza kufanya hivyo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
umebainika kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ilitengua
hukumu iliyotolewa na Mahama ya Wilaya ya Mpanda na
kuamuru wafugaji hao watatu Shigela Mayunga , Charles Mtokambali na
Keleja Makuja warejeshewe mifugo yao pamoja na faini ya Sh
500,000/- walizotozwa .
“Nimesikitishwa sana
na kitendo cha Uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba la Rukwa –
Lukwati kwa kuendelea kuishikilia mifugo hiyo ambapo idadi kubwa ya
mifugo hiyo imekufa kwa magonjwa nataka kujua kwa nini
mifugo hiyo iliendelea kushikiliwa ndani ya hifadhi hiyo huku
eneo hilo likiwa limetengwa maalumu kwa ajili ya wanyamapori na sio
ng’ombe” alihoji Mpina huku akionyesha hisia kali kufuatia ukatili
uliofanywa.
Kwa
upande wake Meneja wa Pori
la Akiba la Rukwa Rukwati
Mhina alieleza kuwa mifugo hiyo ilendelea kushikiliwa
kwa kile alichodai kuwa baada ya
uongozi wa hifadhi hiyo kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Akijitetea
Mhina alisema kuwa ungozi wa hifadhi hiyo ulipewa maelekezo na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kuwa waendelee kuitunza mifugo hiyo kama sehemu ya
kielelezo cha kesi hiyo ..
Akizungumzia
kuchelewa kutekelezwa kwa agizo la Waziri wa Mifugo
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji
Tanzania Makoye Nkonosinema alisema ni kutokana na Mifugo hiyo kuonekana
imeambukizwa Magonjwa baada ya kukosa huduma kwa kipindi kirefu hivyo shughuli
inayoendelea hapo ni mifugo hiyo kutibiwa na madaktari wabobevu ambapo baada ya
shughuli hiyo kukamilika Mifugo hiyo itarejeshwa kwa wafugaji kama Waziri
alivyoagiza.
“Baaada ya uchunguzi wa kina kufanyika,
imeonekana kuwa Mifugo hiyo imeambukizwa Magonjwa na ilikuwa na hali mbaya sana
kiafya baada ya kukosa huduma kwa kipindi kirefu hivyo shughuli inayoendelea
hapo ni mifugo hiyo kutibiwa na madaktari wabobevu kutoka Wizara ya Mifugo
ambapo baada ya shughuli hiyo kukamilika Mifugo hiyo itarejeshwa kwa wafugaji
chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu
wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda kama Waziri alivyoagiza”alisema Mkoye.
Kwa mujibu wa Makoye mifungo mingi
iliyokuwa inashikiliwa hapo imekufa na kwamba Chama hicho kitahakikisha
Serikali inarejesha Mifugo hiyo ikiwa ni pamoja na ongezeko la ng’ombe
wanaodaiwa kuzaliwa lakini idadi inaonekana kubaki kama zilizvyokamatwa Magembe
amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya kutekeleza jukumu alilopewa na Waziri Mpina
mapema.
Mkuu
wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda alipotakiwa kuzungumzia kucheleweshwa
kwa utekelezaji wa agizo la waziri mpina alijibu kwa lugha kali,si uje ofisini?
“mimi nina kikao halafu unaanzaje kuniuliza kutotekelezeka kwa agizo la
waziri? ni agizo lipi? agizo la waziri yupi! na lini? na umejuaje kama waziri
amenipa maagizo? mpigie dc mpanda ndiye aliyetangaza kwenye TV”alisema kasanda
na kukata simu.
Kutokana na hali hii inaendelea
kuonyesha jisnsi baadhi ya wateule Rais Magufuli wanavyoendelea na
kupingana na Sera ya Uhuru na upatikanaji wa Habari kwa wananchi kupitia vyombo
vya Habari kwa kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari pindi
wanapotakiwa kufanya hivyo,ambapo hadi sasa viongzozi hawa wameendelea
kutupiana mpira juu ya nani anatakiwa kutekeleza agizo la Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Mpina.
MWISHO.
No comments: