WASHIKILIWA KWA KUPATIKANA NA BANGI.
Na
Antony Sollo Mwanza.
Watu
wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kwa kosa la kupatikana
na madawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 104.4.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mwanza Dcp: Ahmed Msangi ilisema kuwa tarehe 12.02.2018 majira
ya saa 20:58 hrs usiku katika mtaa wa kiloleli kata nyasaka Wilaya ya Ilemela
Mkoa wa Mwanza, askari wa jeshi la Polisi wakiwa doria walipokea taarifa toka kwa raia wema
kwamba katika mtaa wa Kiloleli kulikuwa na watu waliokuwa wanajihusisha na
uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi.
Baada ya
kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi walifanya upelelezi na msako katika
maeneo hayo nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa shafii abdallah, (21), mkazi wa
Mtaa wa Nyamanoro na John John,(19), mkazi wa Mtaa wa Kitangiri, ambao wanashikiliwa
na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana na bangi kiasi cha gramu 104.4,
kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Taarifa ya Kamanda imeeleza kuwa Shafii abdalah
alikutwa akiwa na bangi yenye uzito wa gramu 38 naJohn John akiwa na bangi
kiasi cha gramu 66.4. ambapo Jeshi la polisi lipo katika mahojiano na
watuhumiwa wote wawili pindi uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa
Mahakamani.
Aidha
msako wa kuwatafuta watu wengine wanaoshirikiana kwa namna moja au nyingine na
watuhumiwa wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya aina ya bangi bado
unaendelea.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa
wakazi wa Jiji la Mwanza hususani vijana kuacha tabia ya kujihusisha na
biashara haramu ya dawa za kulevya kwani
ni kosa kisheria.
Aidha anawaomba
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za
uhalifu na wahalifu mapema ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
No comments: