Wanajeshi wa DRC wamefanikiwa kuwatimua waasi wa M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana
Wanajeshi hao wamekomboa mji wa Bunagana kufuatia makabiliano makali
adhuhuri ya leo ambapo baadhi ya waasi walilazimika kuimbilia msituni
huku baadhi wakidai waliingia Uganda baada ya kuvalia mavazi ya kiraia.
Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.
Wenyeji wa mji huo walithibitishia BBC kuwa mji huo ulikombolewa na kuwa waasi wamekuwa wakitoroka mapambano makali dhidi yao.
Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi
mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23
walianza harakati zao dhidi ya serikali ya Congo mwaka jana wakidaiwa
kusaidiwa na serikali ya Rwanda.
Mnamo siku ya Jumatatu mjumbe maalum wa M23 hawana tena nguvu za kijeshi kwani sio tesho tena.,
Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa usalama wao.
HABARI Na BBCswahili.com
HABARI Na BBCswahili.com
No comments: