Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu: Waziri Mkuu Minzego Pinda Afunga Maonyesho Ya Siku ya Viwanda Afrika
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Bw. George Buchafu wa
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) baada ya kufunga
maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika kwenye uwanja wa Maonyesho wa
Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20,
2013. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dr. Abdallah Kigoda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata
maelezo kutoka kwa Agness Tegete (kulia) wakati alipotembelea banda
la Pani Lihengu Company katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho a
siku ya Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu Novemba 20, 2013
kwenye uwanja wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere,
barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa
Viwanda na Biashar, Dr. Abdallah Kigoda
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara , Dr
Abdallah Kigoda wakati alipofunga maadhimisho ya siku ya Viwanda
Afrika kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya
Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2013. Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Wizara ya Viwanda na Biashara haina budi
kuwaendeleza wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vya kati kwa kuwa
vina mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini.
Ametoa kauli hiyo huo leo mchana (Jumatano, Novemba 20, 2013) wakati
akizungumza na wenye viwanda na wajasiriamali mbalimbali wakati wa
kuadhimisha Siku ya Viwanda Afrika iliyoadhimishwa kwenye Uwanja wa
Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mku alisema sekta
ya viwanda vidogo ina nafasi kubwa sana katika kukuza ajira, kuondoa
umaskini, na kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja na imekuwa ikikua
hatua kwa hatua.
“Hivi sasa sekta
hii ina viwanda vidogo vidogo zaidi ya milioni tatu ambavyo vinaajiri
zaidi ya Watanzania milioni 5.2. Mchango wake katika Pato la Taifa ni
asilimia 27 na kwenye ajira ni asilimia 23.4 ya nguvu kazi yote nchini”,
alisema.
Alisema
msukumo mkubwa uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Nne katika kuendeleza
viwanda ilikuwa ni pamoja na uanzishwaji na uendelezaji wa maeneo ya
fursa huru za uwekezaji kama Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji kwa
mauzo Nje (EPZA) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji (Special Economic Zones – SEZ).
“Serikali
imechukua hatua mbalimbali katika kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi
katika uwekezaji na biashara katika soko la ushindani. Hatua
zilizochukuliwa ni pamoja na kuipa nguvu ya kisheria Mamlaka ya Maeneo
Huru ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA) kusimamia uwekezaji katika
Maeneo Maalum ya Uwekezaji (Special Economic Zones – SEZ).
Katika maeneo hayo, wawekezaji wa sekta mbalimbali wataweza kuzalisha
na kuuza bidhaa katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” alisema Waziri
Mkuu.
Kuhusu usimamizi katika uwekezaji, Waziri Mkuu alisema Serikali
imeendelea kusimamia uwekezaji katika maeneo maalum ya uzalishaji ili
kuharakisha maendeleo ya viwanda. “Uendelezaji wa maeneo ya EPZ na SEZ
ni moja ya mikakati ya kukuza ajira, uwekezaji na uzalishaji viwandani.
Mpango huu una maeneo 10 ambayo yameonyesha mafanikio makubwa yakiwa
yameajiri wafanyakazi 27,000. Miradi yote itakapokamilika, inatarajia
kuajiri wafanyakazi 273,581,” aliongeza.
Alisema
katika kipindi cha miaka sita iliyopita EPZ imeanzisha viwanda 81
katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba viwanda hivyo vimewekeza mtaji
wa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.12 na vimetoa ajira za moja kwa
moja 27,000 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 80,000.
Alisema
mauzo ya nje yamefikia Dola za Marekani milioni 700. Serikali
inaendelea kuimarisha EPZ ili iweze kuwa kichocheo cha kukuza uchumi na
kujenga ajira kupitia maendeleo ya viwanda.
Mapema
akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mku, Waziri wa Viwanda na
Biashara, Dk. Abdallah Kigoda alisema sekta ya viwanda nchini bado
inakua kwa kasi ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.
“Sekta
ya viwanda hapa nchini inakua kwa asilimia tisa wakati China sekta hiyo
imekua kwa asilimia 40, Vietnam imekua kwa asilimi 20 na India imefikia
asilimia 16,” alisema.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na mwakilishi Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Nchini,
Bw. Emmanuel Kalenzi, Mwenyekiti wa CTI, Bw. Felix Mosha na Wawakilishi
wa Jumuiya za Kimataifa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMATANO, NOVEMBA 20, 2013
No comments: